MWINGILIANO WA UTANZU WA MODERN TAARABU- MIPASHO NA MAIGIZO
Mwingiliano wa Utanzu Modern Taarabu- Mipasho na Maigizo
DOI:
https://doi.org/10.14738/assrj.81.9604Keywords:
Mwingilianotanzu; Mwingilianomatini; Taarab; Modern Taarab; mipasho; maigizoAbstract
Muziki wa taarab umepata mabadiliko makubwa na kusababisha kuwepo kwa aina mbili kuu za Taarab: Taarab Asili na Modern Taarab.Utafiti huu ulihakiki mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Malengo ya Makala hii yalikuwa ni kuchanganua miktadha mbalimbali ya mwingiliano tanzu katika muziki wa Taarab ya Mipasho na utanzu wa maigizo na kutathmini dhima ya mwingiliano huo katika muziki wa Taarab ya Mipasho. Makala hii iliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1960) baada ya kuizua kutokana na nadharia ya Mikhail Bakhtin ya Usemezano ambapo imetumika kushughulikia mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Pia nadharia hii imetumika katika kufafanulia uhuru na ubunifu wa mtunzi wa kuingiza vipengele vipya katika kazi. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Ukusanyaji data ulihusisha usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini wa nyimbo za Taarab ya Mipasho ili kupata mistari, vifungu vya maneno na stanza zilizobainisha mwingiliano tanzu. Sampuli ya utafiti ilikuwa nyimbo 32 za muziki wa Taarab ya Mipasho ambazo ziliteuliwa kumaksudi. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulitolewa kwa njia ya maelezo ya kina yaliyohusisha udondoaji na ufafanuzi wa mistari, vifungu vya maneno na stanza zenye kudhihirisha mwingiliano tanzu kutoka kwa data asili. Kutokana na matokeo ya utafiti, mwingilianotanzu mkubwa ulibainika katika uwasilishaji wa muziki wa Modern Taarab ya Mipasho uliorejelewa. Utafiti huu unawachochea wahahakiki wengine wa fasihi simulizi katika kufanya uchunguzi zaidi katika mitindo mingine ya nyimbo za modern taarab kwa misingi ya nadharia mbalimbali za fasihi. Aidha, kutokana na utafiti huu, ilitarajiwa kuwa watafiti wataweza kulinganisha na kulinganua mitindo tofauti ya taarab. Hatimaye, mtafiti anapendekeza tafiti zaidi zifanywe ili miongoni mwa mengine, kusuluhisha mgogoro kuhusu taarab ya mipasho, uwezekano wa kujumuisha nyimbo za taarab miongoni mwa vipera vya utanzu wa nyimbo katika awamu zote za usomi na uhakiki wa fasihi simulizi kwani muziki wa taarab na hasa mipasho bado unahitaji utafiti Zaidi.
